BY ISAYA BURUGU 15TH JUNE,2023-Waziri wa hazina kuu ya kitaifa Njuguna Ndung’u hivi leo alasiri anatarajiwa kuwasilisha bungeni makadirio ya bajeti kwa kipindi cha kifedha cha mwaka 2023/24.Hii ndio bajeti ya kwanza ya utawala wa rais Wiliam Ruto na Waziri Ndungu anatarajiwa kusoma makadirio ya shilingi trilioni 3.6.

Kamati ya kifedha bungeni inapendekeza nyongeza ya shiligi bilioni 80.7  kwenye makadirio hayo huku bajeti yenyewe ikitarajiwa kufikia shiingi trilioni 4.4.

Serikali kuu imetengewa shilingi trilioni 2.2 huku idara ya mahakama ikitengewa shilingi bilioni 22.Kwa upande mwingine bunge la kitaiafa na lile la seneti imetengewa shilingi trilioni 1.6.

Kwa sasa deni la kitaiafa linasimamia shilingi trilioni 9.6 huku serikali  ikitaraji kuomba shilingi bilioni 720.1 zaidi.

 

 

 

 

 

 

 

June 15, 2023