Waziri wa Kawi Davis Chirchir ameonya kuhusu kukatika kwa umeme tena nchini kote ikiwa uwekezaji unaofaa hautaelekezwa katika kuimarisha usambazaji wa umeme kote nchini.

Kulingana na Chirchir, njia za usambazaji umeme nchini zimejaa kupita kiasi, jambo ambalo linaendelea kuzidisha kupotea kwa umeme mara kwa mara.

Chirchir amedokeza kuwa kulikuwa na kizuizi cha usambazaji siku ya Jumapili katika njia ya umeme ya Kisumu-Muhoroni ambayo ilisababisha kukatika kwa umeme kote nchini.

Akikiri kwamba serikali inakabiliana na changamoto za usambazaji wa umeme, Chirchir alisema kuwa njia nyingi za kupunguza zimependekezwa kusaidia kudhibiti kukatika kwa umeme.

 

December 11, 2023