Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ametoa ripoti ya kwanza ya siku mia moja tangu alipoingia ofisini.
Kwa mujibu wa Kindiki ni kwamba kwa siku mia moja, wizara ya usalama wa ndani imefanikiwa kukabiliana na visa vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa katika kaunti ya Turkana.
Ameongeza kuwa wizara hiyo itafanya kila iwezalo kuhakikisha uhalifu na wizi wa ng’ombe umekuwa historia kwa wakaazi wa maeneo hayo.
Hali kadhalika ameeleza kuwa wizara hiyo imeimarisha usalama katika Jiji na kiwango cha uhalifu kimepungua mara dufu.
Waziri huyo vile vile amedai kuwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya maafisa wa usalama katika vikosi vya polisi, uhalifu nchini kote umepungua kwa asilimia 13.5.