Naibu wa rais Rigathi Gachagua na waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki hii leo wamezuru kaunti ya mandera ambapo kongamano la kujadili mikakati ya kiusalama katika mpaka wa Kenya, Somalia pamoja na Ethiopia limeandaliwa.
Kongamano hilo vilevile limehudhuriwa na mawaziri wa usalama kutoka Somalia na Ethiopia pamoja na kamishna wa uingereza nchini Kenya Jane Marriot.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, waziri Kindiki amedokeza kuwa hana shaka kwamba msaada na uungwaji mkono unaokusudiwa kutoka Uingereza utasaidia sana katika kuleta utulivu kwa nchi hizo tatu kukuza biashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha ustawi wa pamoja.
Hata hivyo amezirai Ethiopia na Somalia, kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma kwa kutia saini mkataba wa Usalama uliotiwa saini kati ya Kenya na Uingereza hapo jana.
The Kenya-Somalia-Ethiopia Borderlands Project, a joint venture with support from the UK Government, aims to promote peace and stability in the region and bolster cross-border cooperation.
This project is opportune as the region grapples with complex and sensitive security… pic.twitter.com/C3SoAT9O94
— Kithure Kindiki (@KindikiKithure) May 11, 2023