KINDIKI KITHURE - Radio Osotua

Waziri wa usalama wa Ndani Prof. Kithure Kindiki ameainisha biashara na matumizi mabaya ya pombe haramu na dawa za kulevya miongoni mwa vitishio vikuu vya usalama wa taifa baada ya ugaidi na ujambazi.

Prof. Kindiki ameahidi kuanzisha vita vikali ili kukabiliana na tishio la pombe haramu na dawa za kulevya ambalo anasema ni tishio kwa mustakabali wa nchi.

Waziri huyo alikuwa akizungumza mjini Nyeri wakati wa kongamano la mashauriano la wadau kuhusu tishio la unywaji pombe haramu na dawa za kulevya nchini.

Prof.Kindiki amewataka wadau wote kuungana na kuisaidia serikali katika vita kali dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Kongamano hilo liliwaleta pamoja Maafisa wa Utawala wa Serikali ya Kitaifa wakiwemo makamishna wa kaunti, machifu, wasaidizi wa machifu, Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi, KRA, KEBs na viongozi waliochaguliwa miongoni mwao magavana na Wabunge.

Kongamano sawia na hilo litafanyika Embu, Nakuru, Wajir na Eldoret.

April 14, 2023