Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amesema kuwa wizara hiyo haijawahi toa agizo la kutumia risasi wakati wa maandamano humu nchini.

Akizungumza alipofika mbele ya wabunge, Kindiki ameeleza kuwa Maafisa wote wanaohusika katika kusimamia maandamano ya umma, ghasia na udhibiti wa umati wa watu wako chini ya maagizo makali ya kutotumia risasi za moja kwa moja wakati wa kupambana na umma.

Ameongeza kuwa matukio yote ya mauaji ya kiholela yanachunguzwa kikamilifu, na kudai kuwa seriakli ya rais William Ruto  haitamlinda afisa yeyote anayetumia vibaya bunduki yake kuua watu.

Kuhuasiana na oparesheni ya maliza wahalifu North Rift, Kindiki ameeleza kuwa wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa wahalifu hao wanakabiliwa huku akiwaomba wakenya kuwa na uvumilivu kwani hawawezi wakawakabili wahalifu hao kwa mwezi mmoja.

Aidha ameweka wazi kuwa serikali imeidhinisha maafisa wa polisi wa akiba  200 ambapo 100 watatumwa Baringo kaskazini na 100 waliosalia wataelekea Baringo kusini.

April 12, 2023