Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula amewataka viongozi wa mirengo miwili mikuu bungeni kutafuta njia za kuafikia makubaliano kuhusu jinsi ya kutekeleza mazungumzo ya pande mbili, baada ya mswada kuhusu mazungumzo hayo kuwasilishwa bungeni.

Wetangula alidhibitisha kupokea mswada huo, akieleza kwamba viongozi wa mirengo yote miwili wana jukumu muhimu la kuhakikisha kwamba umoja unaoshuhudiwa nchini unaendelea kutawala. Kauli yake inafuatia taarifa ya viongozi wa Upinzani, waliotishia kujitenga na mazungumzo hayo wakieleza kwamba hawana Imani kuwa yatazaa matunda yoyote.

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka alieleza kwamba mswada huo uliwasilishwa bila nia njema ya kuafikia suluhu.

Kalonzo aidha alieleza kwamba matakwa ya muungano wa Kenya kwanza hayajabadilika kamwe, akisema kwamba mazungumzo yoyote kati yao na serikali yatafanyika nje ya shughuli za bunge na pia lazima mazungumzo hayo lazima yaangazie maswala yote yaliyoorodheshwa na muungano huo.

April 18, 2023