BY ISAYA BURUGU,3RD JULY,2023-Maafisa wa polisi  mjini  Kisumu wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo wezi wanaripotiwa kuvamia   jengo la bunge la kaunti hiyo na kuiba mali ya dhamani ya fedha isiyojulikana.

Katika kisa hicho cha usiku wa kuamkia leo,washukiwa hao waliba runinga zinazotumia kupeperusha   vikao vya bunge  sawa na vifaa vya kuhifadhi data vya mfumo wa hansard.

Kwa mjibu wa karani wa bunge hilo Owen Ojuok,kisa hicho kiliwapata walinzi wa jengo hilo bila ufahamu.Amesema buge hilo lina ulinzi was aa 24 kila siku huku likilindwa na maafisa wa polisi waliojihami na wale wakibinafsi.Owen anasema polisi kwa sasa wanachunguza kisa hicho na watakuwa wakikagua kanda ya kamera za CCTV kubaini jinsi wizi huo ulivyotekelezwa.

Hii si mara ya kwanza kwa bunge hilo kuibiwa,hapo awali,eneo wanakokalia wawakilishi wadi bungeni humo lilivunjwa na vifaa mbali mbali kubiwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

July 3, 2023