Shirikia la chakula duniani WFP, limeupiga jeki mpango wa serikali wa kuwapa lishe mamilioni ya wakenya wanaokabiliwa na makali ya njaa katika maeneo tofauti ya taifa.
Viongozi wa shirika hilo wakingozwa na mkurugrnzi wa WFP humu nchini Lauren Lantis, walitoa ahadi hii baada ya kikao na Naibu wa Rais Rigathi Gachagua Ofisini mwake katika jengo la Harambee alasiri ya leo.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Gachagua ameeleza kwamba shirika hilo limetoa msaada wa Ngano na Mchele Pamoja na misaada mingine isiyo ya vyakula na itakayowasili nchini juma lijalo.
As part of strengthening partnership in responding to drought and famine in the country, I held fruitful discussions with a delegation of the @WFP led by Country Director Lauren Lantis at Harambee House Annex today. pic.twitter.com/hsIHHLDVx7
— Rigathi Gachagua (@rigathi) March 15, 2023