wito umetolewa kwa kina mama kuwa watu wenye sala na upendo katika jamii siku zote.
Akizungumza alipoungana na wanawake kusherehekea siku ya wanawake duniani, msimamizi wa miradi katika jimbo la Eldoret Abigael Mahindu amewataka kina mama kuwa chombo cha sala katika familia zao na kuwa tayari kuonyesha upendo na msamaha kwa kila mtu.
Vilevile amewahimiza wanawake kuwapa wengine matumaini ya kuishi tena kupitia huduma yao ya kujitolea, kuelekeza na kutekeleza majukumu yao kwa bidii ili kupata baraka.
kwa upande wake afisa katika afisi ya haki na amani katika jimbo hilo Laban Gatheiya amewakumbusha kina baba washirikiane pamoja na kina mama katika kutekeleza majukumu yao akitaja kila mtu kushikilia nafasi muhimu katika familia.
Wakati huo huo Kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hivi leo,mama taifa Rachel Ruto aliwatembelea wafungwa wanawake katika gereza la Langa’ta jijini Nairobi.
Bi. Ruto amewahimiza wanawake hao kujitoza kwenye sekta ya ubunifu ili wapate ujuzi utakao wasaidia wanapomaliza vifungo na kurejea nyumbani.