Serikali imejitolea kurekebisha Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya NHIF na kuanzisha mpango mpya wa bima ya afya ya jamii ambayo inakidhi mahitaji ya Wakenya wote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Moyo katika Hospitali ya Coptic, Waziri wa Afya Susan Nakhumicha alisema mpango huo utasaidia kuboresha mfumo wa afya kwa Wakenya kutokana na kubinafsisha gharama za huduma za matibabu.

Wakati huo huo, Kenya inatazamiwa kuzindua kampeni ya kitaifa mnamo Julai 2023, inayolenga kumaliza UKIMWI kwa watoto ifikapo 2030.

June 23, 2023