Zaidi ya vituo vya afya 70 vimefungwa katika kaunti ya Narok kwa kukosa kuafikia viwango vinavyohitajika kisheria kuhudumia wananchi huku watu 6 wakitiwa mbaroni. Hii ni kufuatia zoezi la kukagua hospitali sawa na vituo vyote vya afya kaunti hii.

zoezi hilo liliendeshwa na idara ya DCI kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Narok sawa na baraza la madaktari nchini. Naibu afisa mkuu katika baraza hilo la madaktari na vile vile madaktari wa meno nchini Philip Meeli Ole Kamwaro amesema kwamba kati ya vituo vya afya 255 ambavyo wamefanikiwa kukagua kwa siku tano ambazo zimepita kaunti ya Narok wamefunga zaidi ya vituo 70 kwa kukosa kuafikia viwango hivyo.

Kwa upande wake waziri wa afya katika kaunti hii ya Narok Anthony Namunkuk ametoa shukrani zake kwa baraza hilo la madaktari kwa kazi bora ambayo imefanya sawa na kuleta huduma zake karibu na wananchi wa Narok. Ameshikilia kwamba watashirikiana na baraza hilo kufuatilia wale ambao walitoroka waliposikia ukaguzi unaendeshwa.

November 10, 2023