BY ISAYA BURUGU 23RD JAN 2023-Wanasiasa kaunti ya Narok wametakiwa kujiepusha na malumbano ya kisiasa na badala yake kujihusisha na maswala ya kimaendeleo kaunti ya Narok.Wito huu umetolewa na gavana wa kaunti hii ya Narok Patrick Ntutu.Antony Mintila ana kina cha taarifa hiyo.
Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu amewataka wanasiasa kaunti ya Narok kushirikiana pamoja kubadilisha sura ya mji wa Narok na miji mbali mbali kwa kuinua viwango vya hadhi kimaendeleo. Ntutu amesema serikali ya kaunti ya Narok itafanya kazi na viongozi wote kutoka mirengo mbali mbali kufanikisha miradi za maendeleo kwa wenyeji wa kaunti ya Narok.
Ntutu amesema serikali yake inapania kuleta mabadiliko katika mji wa Narok ili kuepuka mafuriko katika mji wa Narok. Wakati uo huo Ntutu amesema baraza Lake la mawaziri tayari wametwiga jukumu la kufanya kazi kufanikisha maendeleo katika mji wa Narok.
Ntutu amesema serikali itafanya kila juhudi kuhakikisha miundo msingi katika mji wa Narok ni ya kuridhisha. Hayo yanajiri huku malumbano ya kisiasa baina ya gavana wa kaunti ya Narok na seneta Ledama Ole Kina ikishika kazi.